Baada ya kile alichokisema MwanaFA kwa Shirikisho la Muziki Tanzania (SMT) kwa kuwapa saa 48 kuleta jina la Msemaji mpya wa Shirikisho la muziki nje ya Steve Nyerere alieteuliwa wiki iliyopita, kwa kuwa hana sifa ya kupewa nafasi hiyo ikiwemo kutokuwa mwanamuziki, Nay wa Mitego akazia moja kwa moja juu ya maamuzi hayo.
Rappa Nay wa Mitego kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema watu wasimnukuu vibaya MwanaFA na kuongeza kuwa alichosema ni kauli yao na sio ya MwanaFA.
"Kauli ya MwanaFA watu wasiichukulie kama kauli ya KIBABE, KITEMI na kutumia nafasi yake kama Mbunge lakini haya ni mawazo ya Wasanii wengi ambao hawana nafasi ya kuongea na woga wakiamini Steve ni mtu wa Ndani na ana Conection. WENGI Hatuungi mkono maamuzi ya SHIRIKISHO, na hiyo ni kauli yetu sio ya MwanaFA.
Kama mtu Hana SIFA za Uongozi tukikubali atuongoze ni kama tumekubali bora yaende. Yasiwe masaa 48, yawe ata Masaa 24. Steve TUNAKUPENDA kama Msanii wa Kuchekesha lakini sio MSEMAJI na AFISA MIPANGO wetu." - ameandika @naytrueboytz
Ikumbukwe mjadala wa kumkubali na kukataa uteuzi wa Tivu ake ulianzia kwenye mitandao wiki iliyopita ikiwa ni muda mchache tu tangu uongozi wa shirikisho umtangaze.
Post a Comment