Mwanamke wa miaka 59 nchini Uganda achapwa viboko hadharani kwa kufumaniwa akifanya mapenzi na kijana wa miaka 18 😲
Wakazi wanawake wa eneo husika huko Bushenyi kwa muda sasa walikuwa wakimshuku Ms Kedesi Katsigaire(59) kujihusisha kimapenzi na watoto wao wa kiume ambao bado ni vijana wadogo. Ambapo Jumanne iliyopita wakamfuma laivu nyumbani kwake akiwa kitandani uchi na kijana wa eneo hilo mwenye miaka 18 anayeitwa Godfrey Musyotoore
Baada ya hapo waliwapeleka kwenye uongozi wa eneo hilo ambapo kijana husika wa kiume alichapwa viboko 4 kisha kupewa onyo na wazee wa eneo hilo aache mwenendo mbaya
Mwanamke husika nae aliambiwa achague kufanya kazi za kijamii kama sehemu ya adhabu au achapwe viboko 10 ambapo alichagua kuchapwa viboko
Wazee wa eneo hilo wamesema wamemchapa viboko hadharani ili iwe onyo kwa wanawake wengine wenye umri mkubwa wenye tabia za kuharibu watoto
Mmoja wa kiongozi wa eneo hilo amesema suala hilo sio la kisheria sana ila lipo kimaadili zaidi ndio maana wakatoa adhabu hiyo
Tukio limetokea jumaane na baada ya kuchapwa mwanamke husika ametokomea kusikojulikana
Post a Comment