Mpiga debe auawa kisa abiria



Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro linamshikilia mpigadebe wa mabasi ya Abood Abdilah Yassin (32) mkazi wa Kihonda Manispaa ya Morogoro kwa tuhuma za kumuua mpiga debe mwenzake wakati wakigombea abiria kwenye stendi kuu ya mabasi Msamvu.

Kamanda wa Polisi Mkoai Morogoro, Fortunatus Musilim amesema kuwa tukio hilo limetokea machi 28 majira ya saa 12 asubuhi katika stendi kuu ya mabasi Msamvu Manispaa ya Morogoro.

Kamanda Musilim amemtaja aliyeuawa kuwa ni Tazani Mndeme (35) mkazi wa mwembesongo Manispaa ya Morogoro ambaye ni mpiga debe wa mabasi ya BM.

Kamanda Musilim amesema walikuwa wakigombania abiria kwenye stendi hiyo na kwamba wapiga debe hao walianza ugomvi wa kugombea abiria na mtuhumiwa alimchoma kisu marehemu kifuani upande wa kushoto.


 
Amesema mara baada ya kuchomwa na kisu hicho watu waliokuwa kwenye tukio hilo walimkimbiza kwenye hospitali ya Rufaa mkoa wa Morogoro ambapo alifariki wakati akindelea kupata matibabu.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post