Mjue Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa Undani


Rais Vladimir Putin alizaliwa mwaka wa 1952 huko St. Petersburg (wakati huo ikiitwa Leningrad). Baada ya kuhitimu katika Chuo Kikuu cha Jimbo la Leningrad, Putin alianza taaluma yake katika shirika la kijasusi la Russia (KGB) kama afisa wa ujasusi mwaka 1975.

Putin alipanda vyeo haraka katika Serikali ya Russia baada ya kujiunga na utawala wa Rais Boris Yeltsin mwaka 1998, na kuwa waziri mkuu mwaka 1999 kabla ya kuwa rais.

Putin aliteuliwa tena kuwa waziri mkuu wa Urusi mwaka 2008, na mwaka 2012 alichaguliwa kuwa Rais wa Urusi.

Kufuatia kuanguka kwa Umoja wa Kisovieti mwaka 1991, alistaafu kutoka KGB akiwa na cheo cha kanali, na akarudi Leningrad kama mfuasi wa Anatoly Sobchak (1937-2000), mwanasiasa huria.

Katika uchaguzi wa mwisho kama Meya wa Leningrad (1991), Putin alikua mkuu wake wa kitengo cha uhusiano wa mambo ya nje na Naibu Meya wa kwanza (1994).

Baada ya kushindwa kwa Sobchak mwaka 1996, Putin alijiuzulu wadhifa wake na kuhamia Moscow. Mwaka 1998 aliteuliwa kuwa Naibu Mkuu wa Usimamizi katika utawala wa Rais wa Boris Yeltsin, akisimamia uhusiano wa Kremlin na Serikali za Mkoa.

Muda mfupi baadaye, aliteuliwa kuwa mkuu wa Usalama wa Shirikisho, ambalo awali lilikuwa ni tawi la iliyokuwa KGB, na Mkuu wa Baraza la Usalama la Yeltsin.

Agosti 1999 Yeltsin alimfukuza Waziri Mkuu, Sergey Stapashin pamoja na Baraza lake la Mawaziri, na kumpandisha cheo Putin kuchukua nafasi yake.

Desemba 1999 Yeltsin alijiuzulu urais, na kumteua Putin kukaimu nafasi yake hadi uchaguzi rasmi ulipofanyika mapema mwaka 2000. Alichaguliwa tena mwaka wa 2004.

Aprili 2005 alifanya ziara ya kihistoria nchini Israeli kwa mazungumzo na Waziri Mkuu Ariel Sharon, na hiyo ilikuwa ni ziara ya kwanza kwa kiongozi yeyote wa Kremlin.

Kwa sababu ya ukomo wa muda, Putin alilazimishwa kuacha urais mwaka 2008. Lakini alirudi kuhudumu kama waziri mkuu wa Dmitry Medvedevhadi 2012 alipochaguliwa tena kuwa Rais wa Urusi.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post