Jamaa afyekwa kabisa uume wake na mke wake Kisa Hichi Hapa


Mapya yaibuka 😭😭! Jamaa kwa jina la Mr.Nguyen afyekwa kabisa uume wake na mke wake

Tukio limetokea nchini Vietnam wiki hii, sababu ya yote ni jamaa husika kuonesha tabia zisizofaa kwa kumtaka kimapenzi mtoto wa ndugu yake(niece)

Binti husika alilalamikia suala hilo kwa mke wa jamaa, kiujumla binti husika alikuwa anajiheshimu kwahiyo mke akaenda nunua kamera ndogo akaitegesha kitandani chumbani kwa binti bila wote wawili kujua sababu binti alishalalamika zaidi ya mara moja

Tarehe 19 mwezi huu mchana mke akaitazama kamera husika akawa anaona moja kwa moja tabia chafu za mumewe tena kwa mtoto wa ndugu yake kabisa

Baada ya hapo mke alienda kununua kisu chenye makali ya kufa mtu, alimvizia mumewe akiwa kapitiwa na usingizi akamvamia ghafla mithili ya kimbunga kwa kuushika uume wake na kuufyekelea mbali kuanzia kwenye shina lake na kumuacha jamaa akipiga mayowe ya aina yake

Baada ya hapo mke akajipeleka mwenyewe polisi kueleza alichomfanyia mumewe

Mume amepelekwa hospitali lakini madaktari wamemwambia kwa jinsi alivyokatwa ndio basi tena haiwezekani uume wake kupandikizwa tena wala kurudi katika hali ya awali hivyo jamaa kuzidi kuwa na majonzi kwa kuanza maisha mapya bila kiungo chake muhimu


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post