Dully Sykes "Ilibidi Tuachane na STEVE Nyerere Toka Ile Siku Aliyosema Ommy Dimpoz Hata Weza Imba Tena"


Wakati sakata la @stevenyerere2 kuwa msemaji wa shirikisho la muziki/wasanii nchini likiendelea na wengi wakitoa maoni yao,wakiwemo wanaokubali hasa wasanii wa dansi na taarabu lakini pia wanaokataa hasa wasanii wa Bongo Flava, Legend mwenye zaidi ya miaka 23 kwenye game ya B/Flava, @princedullysykes pia ametia neno lake kuhusu ishu hiyo.

Akiwa kwenye Empire ya EFM hii leo March 21, Dully Sykes amedai anamuheshimu sana Steve Nyerere, ila kwenye nafasi hiyo alipaswa kuishia kipindi kile alipogeuka msemaji wa wasanii na kusema @ommydimpoz hatoimba tena baada ya kupata matatizo ya koo, kama wasanii wakamsikiliza lakini cha ajabu Ommy Dimpoz huyu hapa na anaimba vizuri zaidi ya mwanzo. So haoni kama hiyo nafasi ya usemaji inamfaa kwa sasa.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post