Chelsea Yapigwa Kitu Kizito Kichwani, Athari za vita Ukraine



Mzozo wa kivita baina ya Urusi na Ukraine umechukua mkondo mwingine ambao una madhara ya kusikitisha kwa timu ya kandanda ya Chelsea ambayo mmiliki wake ni bilionea kutokea nchini Urusi Roman Abrahamovic anayetajwa na Uingereza kuwa mmoja wa wawezeshaji wakuu wa sera za rais Vladmir Putin.

Mataifa mbalimbali barani Ulaya yanazidi kuiwekea Urusi vikwanzo vikali vya kidiplomasia na kibiashara kwa kile wanachokitaja kwamba ni taifa hilo kukiuka tahadhari za kiusalama na kuivamia Ukraine.

Uingereza pia imemuwekea mmiliki huyo wa Chelsea vikwazo vingi ambavyo moja kwa moja vinaiathiri timu ya Chelsea na shughuli nyingi timuni humo zinatarajiwa kusambaratika huku wadhamini mbalimbali wakijiondoa na wengine kusitisha mikataba yao na timu hiyo ambayo ndio mabingwa wa dunia kwa sasa.


Baadhi ya vikwazo ambavyo serikali ya Uingereza imemuwekea Abrahamovic na ambavyo vina athari hasi kwa timu ya Chelsea ni kuhusu hisa za timu hiyo, uhamisho wa wachezaji ambapo hakutakuwa tena kutia mikataba mipya na wachezaji katika timu hiyo, tiketi za mechi hazitauzwa wala kununuliwa, timu haitaweza kununua wachezaji wapya na pia mmiliki huyo hatoweza kuiuza timu hiyo isipokuwa aishawishi Uingereza kuwa yeye na Urusi hawatofaidi kitu chochote kutoka kwa uuzwaji wa timu hiyo.

Kipengee kingine katika marufuku hiyo kinasema kwamba Abrahamovic ataweza tu kuiza timu hiyo kama ataikubalia Uingereza kuingilia kati na kuwa mmoja wa washikadau wa kuipiga mnada timu ya Chelsea.

Kufikia Alhamis, tayari kampuni ya Uingereza ya Three ilitangaza kukatisha mkataba wa ushirikiano baina ya timu hiyo na kutaka nembo yao kuondolewa kwenye jezi za timu hiyo huku ikisemekana walikuwa wamekaribia makubaliano ya kuongeza mkataba wa miaka miwili na timu hiyo kabla ya mzozo nchini Ukraine.

Mapema wiki iliyopita mmiliki huyo alikuwa amefikia uamuzi wa kuiuza timu hiyo kutokana na marufuku yake aliyokabidhiwa dhidi ya kuingia Uingereza kwa kile mamlaka yqa taifa hilo ilimtaka kuwa mmoja wa wawezeshaji wakubwa wa sera hasi za rais wa Urusi Vladmir Putin.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post