Familia ya muigizaji mkongwe kutoka nchini Marekani Bluce Willis imetoa taarifa iliyoibua simanzi kwa mashabiki wa nyota huyo ikieleza kuwa kuanzia sasa hatoonekana tena kwenye tasnia ya filamu.
Taarifa hiyo inakuja kufuatia nyota huyo kugundulika kuwa ameathirika na maradhi yaitwayo ‘Aphasia’ ambayo yanahusishwa na kuharibika kwa ubongo kunakoweza kusababisha mtu kupoteza uwezo wa utambuzi, kutoa mawazo, hotuba na hata kutoeleweka ipasavyo pindi azungumzapo na hata kuathiri uwezo wa uvumbuzi nk.
“Kwa wafuasi na wapenzi wa Bruce, kama familia tulitaka kushiriki kwamba Bruce wetu mpendwa amekuwa akikabiliwa na matatizo fulani ya kiafya na hivi majuzi amegundulika kuwa na Aphasia, ambayo inaathiri uwezo wake wa utambuzi.
Kama matokeo yalivyo na kwa kuzingatia sana inamlazimu Bruce kuondoka kwenye kazi ambayo imekuwa na maana kubwa kwake, huu ni wakati mgumu sana kwa familia yetu na tunathamini sana upendo wenu unaoendelea, huruma na msaada.
Tunapitia hili kama kikundi cha familia thabiti, na tulitaka kuwaarifu mashabiki wake kwa sababu tunajua jinsi anavyowathamini, kama Bruce anavyosema kila wakati, “Ishi” na kwa pamoja tunapanga kufanya hivyo.”
Imesema taarifa hiyo iliyochapishwa kwenye ukurasa wa mtandao wa Instagram wa mmoja wa watu wa karibu wa Bluce.
Post a Comment