Miamba ya soka nchini Uhispania, vilabu vya Barcelona na Real Madrid viliumana usiku wa kuamkia leo Machi 21, 2022 kwenye mchezo wa La Liga uliochezwa kwenye dimba la Bernabeu na Barcelona kuibuka na ushindi wa 4-0.
Mabao ya Barcelona yamefungwa na Pierre-Emerick Aubameyang aliyefunga mabao mawili, Ronald Araujo na Ferran Torres kila mmoja akifunga bao moja moja na kuzamisha jahazi la Los Blancos kwenye dimba lake la nyumbani.
Ushindi huo umeifanya Barcelona kufikisha alama 54 na kushika nafasi ya tatu ikiwa na mchezo mmoja mkononi baada ya kucheza michezo 28 huku Real Madrid ikisalia kileleni ikiwa na alama 66 na michezo 29, utofauti wa alama 12.
Ushindi huo pia umeifanya Barcelona kurekodi ushindi wake wa kwanza dhidi ya Real Madrid tangu 2019 ambapo walicheza michezo 6 bila ushindi wakifungwa michezo 5 na sare moja ya bila kufungana.
Real Madrid imeambulia kipigo hiko bila ya nyota wake tegemeo Karim Benzema mwenye maumivu ya nyama za mguu na kuwafanya Wababe hao kupokea kipigo kikkubwa katika El Classico kwa mara ya kwanza tangu walipofungwa 5-0, 2009.
Kwa upande mwingine, Mshambuliaji wa Barcelona Pierre Emerick Aubameyang amefunga mabao mawili na kuzidi kufurahia maisha yake Catalunya kwani tayari amefunga mabao 9 kwenye michezo 11 aliyoichezea Barcelona.
Post a Comment