Zamaradi "Bango la Mume Wangu Litakaa Barabarani Mwezi Mzima, Amekuwa Akinipenda Sana"


Zikiwa zimebaki saa chache tu kuingia Valentine’s day February 14 2022 Mtangazaji/Mjasiriamali @ZamaradiMketema ameingia kwenye trend mitandaoni baada ya kutundika barabarani bango lenye picha ya Mume wake likiwa na maneno ‘acha dunia ijue nakupenda kiasi gani, YOU ARE MY KING, happy Valentine’s day my love…… from your loving Wife”

Baada ya kusambaa kwa picha hii @ayotv_ ilimpigia simu Zamaradi ili kufahamu mengine ambapo amesema bango hili ambalo alianza kuliandaa kwa wiki mbili zilizopita bila Mume wake kufahamu, limewekwa leo February 13 saa kumi na mbili jioni na amelilipia litakaa hapo kwa muda wa mwezi mzima "hii ni barabara ambayo anapenda sana kupita yani kila siku lazima apite ndio maana nimeliweka pale"

"Baada ya kuliweka nilimchukua mpaka pale amefurahi sana, tulipofika pale alicheka sana alafu akaingia kwenye gari machozi yakawa yanamtoka akaanza kulia akawa ameinama kwenye gari akasema kwahiyo Mke wangu umeamua kuniweka hapa juu…… amefurahi sana kwakweli”

“Sasa hivi tuna miaka mitano ya ndoa lakini sita ya mahusiano, nia yangu kumuweka kwenye bango ni jinsi ninavyompenda, ninampenda sana Mume wangu, Mume wangu amekua ni Mtu flani ambae amenifanyia vitu vingi hakuna Mtu ambaye anaweza akajua” ——— Zamaradi.

“He is a special man in mylife nafikiri siku moja naweza kukupa Interview ambayo sijawahi kuitoa popote.... amekua ni Mtu ambae ananipenda sana hata maneno hayawezi kutosha kumuelezea ni Mwanaume wa namna gani kwenye maisha yangu" amemalizia Zamaradi. #MapenziMubashara #JamaniRAHA 😃


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post