Baadhi ya Wasanii kutoka makundi mbalimbali ya Muziki leo Februari Mosi, 2022, wameendelea kufika katika ofisi za COSOTA Makao Jijini Dar es Salaam zilizopo, Mtaa wa Kivukoni, Majengo ya Utumishi kwa ajili ya kufanya taratibu za kupata mirabaha yao.
Miongoni mwa waliyofika leo ni Msanii Stamina, Msanii wa Muziki wa Hip pop, Msami Bongo Fleva wa Bongofleva, John Lissu Msanii wa Injili na wengine wengi.
Wakizungumza kwa nyakati mbalimbali na Maafisa wa COSOTA waliipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa kusimamia Hakimiliki za Wasanii na kuwawezesha kupata Mirabaha ambayo kwa muda mrefu walikuwa hawajapata na huku wakisema mgao huo umewatendea haki kwani umeleta uhalisia kwa kuzingatia matumizi ya kazi za Wasanii katika vyombo vya habari.
Pamoja na hayo zoezi hilo la kupokea taarifa hizo muhimu kwa ajili ya kukamilisha mchakato wa malipo ya fedha hizo za mirabaha linaendelea kwa njia ya mtandao kwa wasanii waliopo kazika orodha lakini wasioweza kufika katika ofisi za COSOTA wanaweza kutuma taarifa barua pepe ya group.mirabaha2022@cosota.go.tz
Post a Comment