Vijana Miaka 15 Waongoza Maambukizi ya Ukimwi Tanzania



Vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 24 wanaongoza kwa maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Ukimwi.

Akizungumza mjini Morogoro leo Alhamisi Februari 03/02/2022 Mkurugenzi Muitikio wa kitaifa (TACAIDS), Audrey Njelekela amesema asilimia 50 pekee ya vijana hao ndiyo wana habari kuhusu virusi vya ukimwi.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Auderey, wasichana ndiyo waathirika wakuu katika kundi hilo.

Alisema tafiti zinaonyesha kwamba maeneo ya mjini yanaongoza kwa kuwa na maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU) kwa asilimia 5.5 ukilinganishwa na vijijini yenye 4.2.

Awali ofisa Ufuatiliaji na Tathimini wa Tacaids, Nyangusi Laiser akiwasilisha mada ya hali ya ukimwi nchini alisema idadi ya watu wanaoishi na VVU kufikia mwaka 2021 ni milioni 1.7

Hata hiyo, Laiser alisema maambukizi mapya ya VVU kufikia mwaka 2021 yamepungua kufikia 68,000 wakati vifo vinavyotokana na ugonjwa wa ukimwi vikiwa ni 27,000.

Alisema idadi ya watu wanaofahamu kuwa wanaishi na VVU kwa sasa ni asilimia 84 huku asilimia 98 wakiamtumia dawa za kufubaza VVU (ARVs).

#TimesFmNiBaraka #HatuongeiTunatenda #MgusoWaJamii #FebLove #TimesFMDigital


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post