TCD wafunguka mazungunzo ya Rais Samia, Tundu Lissu



Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT Wazalendo na Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD)
KITUO cha Demokrasia nchini Tanzania (TCD), kimesema mkutano uliofanyika kati ya Rais Samia Suluhu Hassan na Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu, ni hatua muhimu katika kujenga maridhiano ya kitaifa na siasa zenye maslahi kwa wananchi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Alhamisi, tarehe 17 Februari 2022 na Mkurugenzi Mtendaji wa TCD, Bernadetha Kafuko siku moja baada ya Rais Samia kufanya mazungumzo na Lissu, jijini Brussels nchini Ugeliji.

“Mkutano huu wa viongozi wanachama wa TCD ni hatua muhimu sana katika kujenga maridhiano ya kitaifa nchini na kuwezesha kufanyika kwa siasa zenye maslahi kwa Wananchi,” imesema taarifa ya Kafuko

Taarifa ya Kafuko imesema kuwa, mkutano huo utarahisisha kazi za TCD, katika kuchochea matokeo chanya ya kuweka uwanja sawa wa ushindani wa kisiasa Tanzania.


“Mkutano huu pia utarahisisha kazi za kituo kama jukwaa muhimu la majadiliano ya kisiasa nchini, katika kuchochea matokeo chanya ya kuweka uwanja Sawa wa ushindani wa kisiasa hapa Tanzania,” imesema taarifa hiyo.

Aidha, taarifa hiyo imesema TCD inampongeza Rais Samia kwa kufikia hatua hiyo ya kuzungumza na Lissu, ambayo ni matokeo ya mkutano wa wadau wa kisiasa, uliofanyika Desemba 2021, jijini Dodoma, chini ya Baraza la Vyama vya Siasa.




Mkutano huu ambao ni Matokeo ya Mkutano wa wadau wa kisiasa uliofanyika Dodoma Mwezi Desemba 2021 chini ya Baraza la Vyama vya siasa.


“Mkutano huo ni matokeo ya juhudi za viongozi waandamizi wa TCD, katika kuhakikisha kunakuwa na maelewano miongoni mwa vyama wanachama. Umedhihirisha upekee wa siasa za Tanzania,” imesema taarifa ya Kafuko na kuongeza:

“Baada ya mkutano huu tunaamini kuwa sasa wanachama wa TCD vitashirikiana kwani ombi kubwa la wadau muhimu kuonana na Rais limepata jawabu.”

Kwa mujibu wa Lissu, ameutumia mkutano wake na Rais Samia, kumfikishia masuala matano, ikiwemo kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na walinzi wake watatu, Halfan Bwire Hassan, Adam Kasekwa na Mohammed Abdilah Ling’wenya.

Kwenye Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, jijini Dar es Salaam.


Mengine ni zuio la mikutano ya vyama vya siasa vya upinzani, mchakato wa upatikanaji katiba mpya na mfumo mpya wa uchaguzi utakaohakikisha uwepo wa chaguzi huru na za haki.

Lissu amesema, Rais Samia ameahidi kuyafanyia kazi masuala hayo.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post