Sugu "Wadangaji wa Insta Walisema MKE Wangu Mgumba, Tukawajibu Kwa Mimba"


Aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi 'Mr II Sugu' @jongwe__ amewajibu waliomdhihaki kwenye mtandao wa Instagram kwa kumpa mke wake ujauzito baada ya kumsema kwamba ni mgumba.

Sugu amejibu hilo kwenye 'Punchline' ya wimbo wake mpya wa taita aliomshirikisha @billnass baada ya kukaa nje ya game kwa muda mrefu.

"Sina waganga kwangu Mungu ndio muumba, kumbuka wadangaji wa Insta waliposema wife wangu mgumba, hatukuwajibu tukawajibu kwa mimba, leo tuna watoto wanagawana vyumba kwenye mjumba"


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post