Nini Kipo Nyuma ya Watu Maarufu na Kesi za kubaka ?

 


Kwa siku za karibuni kumekuwa na mfululizo wa kesi za kubaka hasa kwa watu maarufu hususani wachezaji mpira na wasanii.

Inawezekana ikawa madai yao ni ya kweli au kuna kitu nyuma ya matukio haya wengi wakihusisha na ile dini inatajwa kuwa ya siri kwamba ukikataa au kuenda kinyume na makubaliano basi ndo wanamaliza na wewe kwa njia hyo.

Baadhi ya mastaa hao ni kama ifuatavyo,

1.CRISTIAN RONALDO: Christian Ronaldo kipindi yupo Manchester United aliwahi kukumbwa na kashfa hyo ila ikapotea ikaja kuibuka tena siku za karibuni ila ikapotea bila kwenda mahakamani.

2.KARIM BENZEMA : Karim benzema na yeye ni miongoni mwa watu waliowahi kuwa na skendo kama hiyo iliyomfanya akawa nje ya timu ya taifa kwa miaka mitano.

3.ROBINHO: mchezaji wa zamani wa Manchester city na team ya taifa ya Brazil na yeye ni miongoni mwa watu maarufu walio pata kashfa kama hyo na kuhukumiawa kwenda jela.

4.BENJAMIN MENDY: Mchezaji wa Manchester city na team ya taifa ya ufaransa kwa siku za karibuni zimeibuka taarifa za yeye kubaka na club yake kusitisha mkataba nae ila kesi yake bado inaendelea.

5.R KELLY: Msanii mkongwe kutoka marekani ambaye alihukumiwa kwenda jela kwa kosa la kutembea na binti wa chini ya umri wa miaka 18 ambayo wahusika walidai walijaribu kufuatilia madai yao kwa miaka 20 bila kusikilizwa.

Nadhani humu ndani kuna watu wajuzi na wakongwe,

Je ni kweli wanabaka au ni kesi za mchongo na kwa nini wengi ni watu weusi tu wanaukutwa na hatia.

Wasalam.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post