MWALIMU wa shule ya msingi aliye na umri wa miaka 34 ameshtakiwa kwa kula asali ya mwanafunzi wake.
Hakimu mwandamizi Esther Bhoke alifahamishwa tayari mwanafunzi huyo yuko na mimba iliyo na miezi mitano. Silas Omoro Okwaro ameshtakiwa kutekeleza uhalifu huo kati ya Juni na Oktoba mwaka uliopitaq kinyume na sheria za ngono zilizopitishwa 2006.
Mshtakiwa alikiri shtaka lakini akabadilisha nia alipoelezwa atasukumwa jela maisha ama kifungo kisichopungua miaka 20. Alikabiliwa na shtaka la ubakaji na kumdhulumu kimapenzi mlalamishikwa kushikasehemu zake nyeti. Okwaro alidaiwa alimchafua msichana huyo ndani ya darasa katika kituo cha Shamma Children’s Centre kilichoko mtaa wa mabanda wa Kibera, Nairobi.
Mshtakiwa anayefundisha somo la isabati alidaiwa ameshiriki ngono na msichana huyo kati ya Juni na Oktoba 2021. Mlalamishi alidaiwa alikuwa anamtembelea mwalimu huyo katika makazi yake kuponda raha baada ya wao kukubaliana kuwa marafiki.
Mlalamishi alizirai akiwa shuleni kisha akapelekwa hospitali ilipotambuliwa ni mja mzito.Okwaro aliachiliwa kwa dhamana na hakimu mwandamizi Bi Esther Bhoke ya Sh300,000 na mdhamini mmoja wa kiasi hicho. Bi Bhoke aliamuru kesi itajwe tena Feburuari 22 kwa maagizo zaidi.
Post a Comment