Hatimaye Mange Kimambi Afunguka Sababu za Kumuita Mama Marehemu Dr Mwele Malecela "Hamuwezi Kuelewa Alinipenda"


Reposted from @mangekimambi_ PART 1. Maswali yamekuwa mengi kama Dr. Mwele alikuwa ni mama yangu mzazi au vipi? Kwangu mimi haina tofauti kama alinibeba tumboni kwake au la, sababu mapenzi aliyonipa hayana tofauti naya mama mzazi. Her love for me was UNCONDITIONAL. Na matatizo yangu yooote na lawama zooote nilizokuwa namletea hakuna siku aliwahi kuniacha au kuniambia nimekuchoka. Sometimes nilikuwa nikifanya tukio naogopa hata kumuona maana sijui atasema nini ila nikimuona ndo kwanza atanipa mapenzi utasema I’m that perfect unproblematic daughter wakati I’m just the opposite of that. Hata ningeua nahisi bado angenipenda. Sijui kama kuna kitu ningefanya hapa duniani kikafanya akaacha kunipenda. UNCONDITIONAL LOVE niliijulia kwake…



Kabla baba yangu hajafariki alinikabidhi kwa Dr. Mwele. Alimwambia kuwa akifa watoto wake wooote watakuwa sawa Mange ila hana mtu, naomba usimwache Mange. Naomba umwangalie. Naomba uhakikishe anasoma anamaliza mpaka na yeye aje kuitwa Dr. kama wewe. Yes, dream ya baba yangu ilikuwa nipate PhD niitwe Dr. Kimambi. Alikuwa ananiambia unamuona Dr. Mwele anaitwa Dr. Malecela na wewe lazma uitwe Dr. Kimambi. Baba yangu hakuhabatika kupata elimu basi alikuwa ana admire sana watu wenye elimu kubwa. Yani kilichomu attract baba yangu kwa Dr. Mwele ni intelligence yake, elimu yake na ile power of a self made woman. He was so proud of her. Alikuwa hajawahi kuwa na mwanamke mwenye akili kubwa vile. My dad respected Dr. mwele so much.


Bila Dr. Mwele degree yangu nisingemaliza, hata master yangu nisingeifanya. Alikuwa ananipush kwenye issue ya elimu. Nakumbuka siku ya graduation yangu ya masters nilikuwa nafurahi sana nasema sasa nimemalizana na vitabu akasema, umemaliza wapi wakati mimi na wewe wote pamoja tulimuahidi baba yako utaitwa Dr. Kimambi? Nkamwambia ila mama ujue baba alisema issue ni kuitwa Dr. Kimambi, vipi nikitafuta hata udoctor wa mitishamba? Alichekaaaa, OMG she had the most infectious laugh. I will miss her laugh. Haki alikuwa na kicheko flani akicheka na wewe lazma ucheke. Yani anacheka hadi anakaukia. The most beautiful laugh I have ever heard in my entire laugh.

Mnakumbuka niliwapaga ile story ya kwamba step mom wangu alinyima school fees nikaiba

Reposted from @mangekimambi_ PART 2. gari home niende kuuza vipande vipande nipate school fees? Basi ile siku nafanya lile vagi home Dr. Mwele alikuwa keshanilipia school fees. Nilivyomwambia tu nimenyimwa school fees, aliniambia njoo kesho tuongeee, naenda ananipa bahasha lina school fees ya mwaka mzima na pocket money juu. Akaniambia rudi hostel usome. Shule utashindwa wewe ila hata iweje nitakulipia. Uwiii, nililiaaa, sikuamiini kanipa school fees hata sijamuomba na kilichoniliza sio tu kunipa fees ila sababu alikuwa tayari analipa school fees za watoto wengine kama 10 au zaidi na hapo kwake tayari kuna watoto karibia 10 anaishi nao alafu bado anajiongezea mzigo wa kunilipia mimi school fees. Roho iliniuma nikasema hapana sitokuwa mzigo kwa huyu mama. Ndo nikaenda kufight mpaka nikapewa school na msimamizi wa mirathi nikamrudishia Dr. Mwele akaniuliza umetowa wapi hela? Ndo nampa story ya kuiba gari na kutafutwa na polisi etc mpaka kupewa pesa. Alibaki kaduwaaa akasema mwanangu drama za nini pesa sinilishakupa? nkamwambia hapana mama baba alisema unisimamie nisome hakusema unisomeshe kuna tofauti kubwa hapo, pesa za mimi kusoma baba kaacha na ntazipata sitaki kuwa mzigo kwako, woote wawili tukaanza kulia. Na aligoma kuzipokea pesa nilizomrudishia akasema hizo kaweke kwenye bank siku ukipata tena matatizo utatumia hizo kulipa school fees. Yani sikuamini nilibaki nalia tu, namuuliza kwanini ananipenda hivi wakati babangu alishakufa anafaidika na nini kunipenda mimi? Alafu mimi mkorofi hakuna mtu duniani anaweza kunipenda moja kwa moja lazma achoke tu? Akaniuliza baba yako na mama yako walikuchoka? Nikasema hapana, akasema sasa na mimi si mama yako? Naanzaje kukuchoka, kwani nilikuwa sikujua ukorofi wako wakati namkubalia babako kukulea?

Dah!! Dr. Mwele hakuwa binadamu kama sisi , yule alikuwa malaika alieletwa duniani kwenye mwili wa binadamu.Na sio mimi tu naweza kusema hivi. Hivi mnajua nyumba ya Dr. Mwele ilikuwa inajaa watoto wa ndugu, jamaa na marafiki zaidi ya 10 24/7? na hapo ni anawalisha anawavisha na kuwasomesha, yani hamuwezi kuelewa.." Mange Kimambi


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post