Covid-19: Utafiti Waonyesha Kafyu na ‘Lockdown’ Hazikuwa na Umuhimu



Covid-19: Utafiti waonyesha kafyu na ‘lockdown’ hazikuwa na umuhimu
NA MARY WANGARI

WANASAYANSI wanataka masharti ya kudhibiti Covid-19 kutupiliwa mbali.

Hii ni baada ya utafiti kuonyesha hatua zilizochukuliwa mwanzoni zilikuwa na athari ndogo au hazikuwa na umuhimu wowote katika kukabiliana na janga hilo.

Kulingana na utafiti huo ulioongozwa na wataalamu wa Chuo Kikuu cha Johns Hopkins nchini Marekani, masharti ya kufunga mipaka haikuwa na athari yoyote katika kupunguza vifo vilivyotokana na Covid-19.

Matokeo hayo yanasema mikakati iliyowekwa mnamo 2020 kufuatia kuzuka kwa Covid-19 ikiwemo kafyu, kuvalia maski na kudumisha umbali ilipunguza idadi ya vifo kutokana na gonjwa hilo kwa asilimia 0.2 pekee.


Hatua ya kufunga shule nayo ilipunguza idadi ya vifo kutokana na virusi vya corona kwa asilimia nne.

Hata hivyo, hatua ya kufunga vituo visivyotoa huduma muhimu ilitajwa kama mikakati bora zaidi iliyoongoza kwa kupunguza idadi ya vifo kutokana na Covid-19 kwa asilimia 10.6.

Watalaamu hao wamefafanua kuwa matokeo ya utafiti huo huenda yalitokana na masharti ya kufunga vilabu na mikahawa ambapo watu hubugia pombe.


Kafyu ya kutotoka nje usiku hapa Kenya ilidumu tangu Aprili 2020 hadi Oktoba 2021.

Serikali pia mara kwa mara iliweka maeneo ya kuingia na kutoka baadhi ya maeneo.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post