Country Boy Atoboa Siri "Niliruhusiwa Kutoa Ngoma Mbili tu Kwa Mwaka Pale Konde Gang"



Wakati Harmonize ametoka kukamilisha ziara yake ya muziki huko kwenye ma nchi ya wenzetu, alipotua Airport aliongea mambo mengi kuhusiana na alichokuwa akifanyiwa na uongozi wake wa zamani (WCB)

🍁Moja ya vitu aliongea ni mkataba ulikuwa ukimruhusu kutoa nyimbo mbili tu kwa mwaka lakini pia mapato yaliyokusanywa kupitia muziki wake alikuwa anachukua (40%)

🍁Sasa Baada country boy kutoka KONDEGANG amefanya interview na @millardayo na kufunguka mambo yale yale ambayo harmonize aliongea akiwa pale Airport kuhusiana na mfumo wa kutoa ngoma (idadi) na (malipo)

🍁Country boy amesema alikuwa akiruhusiwa kutoa ngoma mbili tu kwa mwaka pia baada ya makusanyo ya mapato kutokana na kazi yake ya mziki yeye alipata (45%)

🍁Najiuliza kulikuwa na haja gani kwa Harmonize kuongea yote yale wakati pia mikataba ya KONDEGANG haitofautiani sana na WCB?

🍁Isitoshe country boy hakuwa anapewa promotion kubwa hivyo kusababisha upatikanaji wa pesa ndogo na bado anachukua (40%) tu. Monthly listeners wa country boy kwa upande wa spotify ilikuwa ni 2500 ikizidi ni kidogo tu.




0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post