Bernard Morisson Asamehewa Simba, Aonekana Kwenye Mazoezi



Kiungo Mshambuliaji wa Wekundu wa Msimbazi Bernard Morrison, ameruhusiwa kurejea kikosini leo baada ya kumaliza kesi yake ya utovu wa nidhamu iliyokuwa inamkabili.

Siku chache zilizopita Morrison alituhumiwa kwa makosa ya utovu wa nidhamu ambapo alisimamishwa kwa muda pamoja na kutakiwa kutoa maelezo kwa Mtendaji Mkuu wa Klabu Barbara Gonzalez.

Morrison aliomba radhi kwa uongozi na benchi la ufundi na mapema leo alifika katika ofisi za Klabu na kuwa na maongezi na Mtendaji Mkuu Barbara.

Taarifa za uhakika zinadai kuwa katika maelezo yake Morrison ameomba radhi na ameahidi kutorudia makosa. Taarifa zinasema Morrison ameshawasili kambini Jioni ya leo na amefanya mazoezi katika Uwanja wa Mo Arena Uliopo Bunju.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post