Tangia watakoma nimekuwa ni mtu ambae naamini sana kipaji cha @iamamberlulu ,anajua sana kuimba na ana vitu vyake ambavyo vinakufanya uendelee kusikiliza ngoma zake. Kwa bahati mbaya ni msanii ambae ikitajwa list ya wasanii wa kike wanaofanya Bongo Flava unaweza usimkute sababu bado hajawekwa kwenye picha ya wanamuziki hapa nchini.
Niliwahi andika na nitaendelea kuandika kuhusu vipaji vya hawa watu, Gigy Money na Amber Lulu, nawaona wana pesa zao nzuri kwenye huu muziki, ila bado sijajua tatizo liko wapi. Ukipewa playlist yenye nyimbo tupu za Amber Lulu, unaweza ukaskip wimbo mmoja au mbili lakini zinazo baki zote zitakuhitaji uzisikilize.
Halichachi ft Kayumba ni wimbo ambao umefanya leo niandike tena kuhusu Amber Lulu, wimbo mkali sana kwenye kila kitu,ila bado Media kama haziupeleki unapotakiwa. Hawa viumbe wanahitaji sapoti yetu kwenye muziki wanaofanya na sio picha wanazo post kwenye mitandao yao ya kijamii.
Unahisi kipi kinamkwamisha Amber Lulu kwenye hili game?
Post a Comment