Wanamuziki mahiri wa muziki wa Bongo fleva kutoka WCB Zuhura Othman maarufu Zuchu pamoja na Mbwana Yusuf Kilungi maarufu Mbosso wamefanikiwa kuingia kwenye orodha ya vijana 100 wenye ushawishi mkubwa zaidi barani Afrika kwa mwaka 2021.
Hii ni kwa mujibu wa Evance Media kutoka nchini Ghana ambao wamechapisha taarifa hiyo kwenye mtandao wakiambatanisha na orodha ndefu yenye jumla ya vijana 100 kutoka mataifa mbali mbali barani Afrika.
Katika orodha hiyo wamo waigizaji, wachekeshaji, Wafanyabiashara, wabunifu wa mavazi, wanamitindo na wengine wengi.
Wengine waliotajwa kwenye orodha hiyo ni pamoja na wasanii kutoka nchini Nigeria akiwamo Tems, Burna Boy, Davido, Wizkid, Joe Boy pamoja na Facolistic kutoka Afrika kusini.
Post a Comment