Wezi wawili wa Nairobi wanaugulia maumivu ya risasi za mguu Hospitalini mida hii baada ya kuwaibia simu Askari Polisi ambao hawakuwa wamevaa kipolisi kwa kuikwapua kwa kuwavizia wakiwa kwenye foleni ya magari eneo la Allsopps Nairobi Kenya jana.
Wawili hao walipigwa risasi za mguu kila mmoja baada ya kuiba simu ya Inspekta Elizabeth Lumumba na kukaidi amri ya kusimama baada ya kumuibia Inspekta huyo ambaye alikuwa amebebwa na Koplo Hassan Mbwana kwenye gari binafsi.
Imeelezwa baada ya kumuibia Inspekta huyo Wezi hao waliendelea kuwaibia Watu wengine waliokuwa wamekwama katika foleni ya magari na ndipo Inspekta Lumumba pamoja na Polisi mwingine aliyekuwa kwenye gari waliposhuka na kuwapiga risasi kwenye mguu baada ya kukaidi amri ya Polisi hao iliyowataka kusimama.
Post a Comment