Wafungaji Wanaoongoza kwa Mabao Ligi Kuu Mpaka Sasa



Dalili za ubingwa zinanukia mitaa ya Jangwani ambapo mpaka sasa klabu hiyo imekua imara sana karibu maeneo yao yote ya yaani kuanzia eneo la ulinzi hadi eneo la ushambuliaji ambalo linaongozwa na mshambuliaji hatari Fiston Mayele raia ya Kongo.

Katika kuhakikisha kwamba tunalinda kumbukumbu na takwimu za wachezaji wa klabu hii bora msimu huu, chanzo cha kuaminika cha takwimu za wachezaji kimetoa orodha ya wachezaji wenye magoli mengi ndani ya kikosi cha Yanga baada ya timu hiyo kucheza jumla ya michezo 13 ya NBC Premier League.

Kwa mujibu wa chanzo hicho ni kwamba mshambuliaji tegemezi wa klabu ya Yanga kwa sasa Fiston Mayele anaongoza katika orodha baada ya kufunga magoli 6 kwenye michezo 6 ya NBC Premier League msimu huu.

Mayele licha kuongoza katika orodha ya wafungaji bora ndani ya kikosi cha Yanga lakini pia nyota huyu anashikilia nafasi pili kwenye orodha ya wafungaji bora ndani ya NBC Premier League ambapo kwa sasa mfungaji nambari moja ni R. Lusajo wa Namungo Fc.


 
Viungo washambuliaji wa klabu ya Yanga Feisal Salum na Saido Ntibazonkiza wanashikilia nafasi ya pili katika orodha ya wachezaji wenye magoli mengi ndani ya klabu ya Yanga baada ya kufunga magoli manne kwenye michezo 13 ambayo Yanga wamecheza mpaka sasa.

Saido na Feisal ndio wanaofanya kazi kumtengenezea Fiston Mayele nafasi za kufunga magoli lakini pia wanafanya jitihada za wao wenyewe kufunga magoli mengi kadri iwezekanavyo ili angalau kuwasogeza Yanga kwenye nafasi nzuri ya kutwaa taji la ligi msimu.

Yanga wamekua bora sana msimu huu na hii inaonyeshwa na namna ambavyo washambuliaji wa timi hii wanavyopambana kuhakikisha kwamba wanavuna alama tatu katika kila mchezo wanaocheza.


Takwimu hizi zinaonyesha wazi kwamba washambuliaji watatu wa klabu ya Yanga yaani Mayele, Feisal na Saido wamehusika kwenye magoli 14 ya kufunga wakiwa na kikosi cha Yanga msimu huu ambao ni M
magoli mengi kuliko safu za washambuliaji wa timi nyingine zinazoshiriki ligi kuu msimu huu.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post