Ukistaajabu ya Harmonize na Briana Basi Utashangaa ya Rayvanny na Paula


Ikiwa ni siku chache tu tangu mwanamuziki harmonize atembeza Unfollow kwa mpenzi wake mzungu #Briana ghafla tu na kisha kutangaza kuwa yupo single, jambo ambalo lilichukua attention ya watu kabla ya badae kukanusha taarifa hizo nakisha kuachia ngoma.

Sasa jambo hili huenda likawa Copy & Paste au likawa linajirudia kwenye couple nyingine ya star wa muziki #Rayvanny na mpenzi wake #Paula baada ya wote wawili ku futana urafiki katika mtandao wa Instagram, na kutoishia hapo wamefuta pia picha zote walizowahi kupiga wakiwa pamoja ,huku kila mmoja akiwa hajazungumza chochote kuhusu hilo.

Maswali yamekua mengi kuwahusu kama Je wawili hao wameachana? Au ndo kama yake ya Harmonize na Briana..? Lakini pia hili limekua likihusishwa na ujio wa EP ya flowers II , ambayo Rayvanny ametangaza kuwa itatoka hivi karibuni, katika kipindi cha wapendanao.

Ukistaajabu ya Harmonize & Briana, Utayaona ya Paula na Rayvanny, huo ndio msemo wa kihenga ambao pengine ungefaa kutumika katika kipindi hiki.

C©✍🏾@keviiiy.iam




0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post