Hatimaye Lile Gari Ambalo Linaloweza Kubadilika na Kuwa Ndege Ndogo Limefaulu Majaribio


Hatimaye lile Gari ambalo linaloweza kubadilika na kuwa Ndege ndogo limefaulu majaribio ya safari za ndege nchini Slovakia, Watengenezaji wa gari hilo wamethibitisha na kusema gari hilo limetunukiwa rasmi cheti na Mamlaka ya Usafiri Nchini humo baada ya kufikisha saa 70 za majaribio (dakika 4200) angani.


Cheti hiki sasa kinaipa nguvu kampuni iliyotengeneza magari haya kuanza kuyaingiza sokoni kwa ajili ya kuyauza ambapo moja ya masharti kwa Mnunuzi yeyote ni lazima awe na leseni inayotakiwa ili kuruka na gari angani, tayari imeshafahamika kwamba magari haya ya "AirCar" yataingia sokoni kuanza kuuzwa kibiashara December 2022.




0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post