BASATA wavianika vipengele vya Tuzo za Muziki Tanzania 2021, hivi hapa, watoa siku 3 kupokea maoni




Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limetoa siku tatu kwa wadau wa muziki nchini kutoa maoni yao juu ya vipengelee (Categories) vya tuzo za muziki Tanzania 2021.


Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mtendaji wa baraza hilo Matiko Mniko wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika Makao Makuu ya ofisi zilopo Kivukoni Jijini Dar es Salaam.


Aidha Mniko amevitaja vipengele vitavyoshindaniwa katika tuzo hizo na kueleza kuwa Kuna Vipengele 23 na ndani yake Kuna jumla ya tuzo 52.


Tuzo hizo zilizozinduliwa Januari 28 mwaka huu na Waziri wa utamaduni Sanaa na michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa Jijini Dar es Salaam zinatarajiwa kutolewa 26 March 2022 baada ya washindi kupatikana kutokana na kura zitakazopigwa na wadau wa muziki kwa njia ya mtandao..


Kwa maoni yoyote tuma kupitia Barua pepe:

info@basata.go.tz




2 Comments

Post a Comment

Post a Comment

Previous Post Next Post