Afisa wa Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Greyson Mahembe ambaye ni miongoni mwa maafisa saba wa jeshi hilo waliofunguliwa mashtaka ya mauaji ya mfanyabiashara amejinyonga kwa tambala la kudekia akiwa mahabusu ya kituo cha polisi wilaya ya Mtwara.
Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara liliwakamata na kuwafikisha mahakamani Maafisa wa Polisi saba kwa tuhuma za mauaji ya Mussa Hamisi Hamisi (25) mkazi wa Kijiji cha Ruponda wilayani Nachingwea Mkoani Lindi aliyekuwa akiwadai askari hao zaidi ya Sh milioni 33.7.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Marck Njera ilisema mauaji hayo yalifanyika Januari 5, 2022 na mwili wa marehemu ulitupwa kitongoji cha Majengo kijiji cha Hiari Wilayani Mtwara
Post a Comment