Msanii Zuchu ni miongoni mwa wasanii ambao wamesajili katika lebo ya WCB inayomilikiwa na staa wa bongo Diamond Platnumz.
Baada ya kujiunga na lebo hiyo Zuchu ameonekana akiinuka kutoka kiwango kimoja hadi kingine kutokana na biii yake.
Ni msanii ambaye ana uhusiano mwema na wa karibu na Diamond, kama inavyoonekana mitandaoni.
Licha ya kejeli zote ambazo Zuchu amepokea kutoka kwa wanamitandao, amezidi kutia bidii kila kuchao.
Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram msanii huyo alipakia video huku akionyesha nyumba yake na kusema kwamba alikuwa ameithamini.
Pia aliweka wazi kwamba yuko tayari kusherehekea sikukuu ya krismasi, na hata kumshukuru Diamond kwa umbali amemtoa.
" Mimi Dai akinipata sikuwa na chochote . Alinikuta maskini akanitunza kama Mtoto wake. Alinipa mkataba katika Lebo yake, akanipa nyumba , akanipa gari na kunitafutia umaarufu unaonilisha Leo hii. Dai ni zaidi ya babangu Allah azidi kumueka poa Kwa ajili ya wengine wengi," Alisema Zuchu.
Post a Comment