WIKIENDI iliyopita mwanamitindo wa kimataifa wa Bongo, Hamisa Mobeto aliteka mazungumzo mtandaoni baada ya mahaba yake mazito na rapa wa Marekani, Rick Ross kisha akatua Bongo na kufunguka mazito juu ya uhusiano wake na mwamba huyo.
Rapa huyo ambaye jina lake halisi ni William Leonard Roberts II, alijizolea umaarufu Afrika kupitia nyimbo mbalimbali ikiwemo Sorry, Money Dance, The Devil Is A Lie na ule wa Beautiful Onyinye alioshirikishwa na Kundi la P-Square la Nigeria.
Hivi karibuni Rick Ross au Boss alijikuta midomoni mwa Wabongo baada ya kuonekana akiwa anatoa maoni kwenye posti mbalimbali katika ukurasa wa Mobeto huku baadhi wakisema kuwa tayari wawili hao wapo kwenye uhusiano wa kimapenzi.
Wakati watu wakidhania hivyo, gazeti hili la IJUMAA WIKIENDA lina habari za ndani kabisa kwamba ukaribu wa Mobeto na Rick Ross unatokana na wao kuwa mabalozi wa kutangaza kinywaji maarufu duniani hivyo kujiita familia, lakini hakuna mapenzi kati yao na hata walipokutana kwa mara ya kwanza Dubai hawakulala pamoja.
MENEJA WA MOBETO
Juni, mwaka huu, gazeti pacha la hili la IJUMAA lilifanya mahojiano maalum na meneja wa Mobeto, Dk Ulimwengu ambapo alipouliza kuhusu jambo hilo kama lina ukweli, majibu yake ilikuwa ni tusubiri hapo baadaye kuona kinachoendelea kwani ni mapema sana kulizungumzia suala hilo.
Alipoulizwa kama Mobeto ana uhusiano wa kimapenzi na Rick Ross, alisema hawezi kuzungumzia jambo hilo kwa kuwa huwa hausiki na uhusiano wa mrembo huyo na hayo ni maisha yake binafsi yeye anachodili naye ni ishu za kazi tu.
MANENO YA RICK ROSS
Hata hivyo, Septemba, mwaka huu akihojiwa katika Podcast ya Lil Ommy, Rick Ross alisema yeye na Mobeto wana ukaribu aliyouita connection, huku akimtaja kama mjasiriamali mkubwa ambaye anataka kumsaidia ili afike mbali zaidi.
“Well, I have to be honest. There is a connection. There is. Oh yeah. How much Imma tell you about it? Imma leave that to her,” alisema Rick Ross na kuongeza;
“So, I want you to make sure you do an interview and you do it with her but she is such a beautiful person, a beautiful spirit and she is a huge entrepreneur and I know I want to help her take it to the next level because she’s doing a great job and I’m proud of her but it is a lot, it’s a lot of things for her to accomplish and a lot more money to get and I want to see her win.”
MOBETO ATUA, AVUNJA UKIMYA
Juzi, Mobeto alitua jijini Dar akitokea Dubai na kuvunja ukimya juu ya uhusiano wake wa kimapenzi na Rick Ross; mmoja wa mastaa matajiri zaidi duniani;
“Kama kutakuwa kuna kitu chochote kinachoendelea mtafahamu, mimi naendana na mtu yeyote yule nikikaa naye karibu, sema tu sinaga desturi ya kuonekana na wanaume public ndiyo maana inaonekana hivyo, lakini tunapendezana, wote tukiongozana hivi…”
“Nimeenda Dubai kwenye biashara zangu pia Rick Ross ana mpango wa kuwekeza Tanzania, ana mpango wa kuifanya Tanzania kuwa second home yake, amemtaja mpaka Rais wetu Samia na mimi ni Mtanzania kama kutakuwa na kitu chochote cha ziada nitawaambia.
HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE
“Mimi nina bahati ya kukutana na wasanii wa nje wengi na kuwa karibu nao ni rahisi kwangu wapo ambao nimekutana nao sijapiga picha, uhusiano wangu na Rick Ross ni kwa sababu nafanya kazi naye, ni mara ya kwanza kumuona he is so amaizing, ni gentleman, sisi kuondoka pamoja club siyo ishu mwanaume anatakiwa am-take care mwanamke.”
Post a Comment