Wakamatwa JNIA kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya




Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kikosi cha Viwanja vya ndege vya Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) imewakamata wanaume wawili watanzania wakiwa na pakiti saba za dawa za kulevya aina ya Heroin zenya uzito wa kilo 7.116 walizokuwa wameficha ndani ya mabegi ya nguo zao

Kamanda wa Polisi wa  Viwanja vya ndege Tanzania,Jeremia Shila alisema Novemba 25,2021 saa 5 asubuhi eneo la kuwasili abiria toka nje ya nchi walikamatwa watuhumiwa hao jengo la abiria.

Shilla alisema watuhumiwa hao walikamatwa baada ya kuwasili na ndege ya Fly Dubai yenye namba ya mruko FZ 1687 wakitokea Ahmedabad nchini India kupitia Dubai .

Alisema mtuhumiwa wa kwanza mwenye umri wa miaka 45 mkazi wa Mbagala jijini Dar es Salaam alikamatwa na pakiti tano za dawa za kulevya aina ya Heroin zenye uzito wa kilogramu 3.266 alizozificha ndani ya begi lake la nguo


 
Shila alisema mtuhumiwa wa pili mwenye umri wa 42 Mkazi wa Tabata jijini Dar es Salaam alikamatwa akiwa na pakiti mbili za dawa ya kulevya aina ya Heroin zenye uzito wa kilo 3.85 alizoficha ndani ya begi lake la nguo.

""Watuhumiwa hawa walikamatwa kutokana na umahiri wa askari polisi wa JNIA wakishirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama vilivyopo uwanjani hivyo upelelezi unaendelea utakapokamilika watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani"alisema Shila.

Shilla alitoa onyo kali kwa watu wanaojihusisha na biashara haramu ya kusafirisha dawa za kulevya kwa kuwa watakamatwa na kuchukuliwa hatia kali za kisheria.


Pia alisema wamejipanga vizuri ndani pamoja na maeneo mengine yanayozunguuka Viwanja vya ndege vya JNIA dhidi ya matukio mbalimbali ya kihalifu hasa kuelekea  sherehe za uhuru, Krismass na mwaka mpya.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post