BERNARD Morrison, kiungo mshambuliaji wa Simba ya Tanzania, amejinyakulia tuzo na Sh.2 milioni, baada ya kuchaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mashabiki wa mwezi Novemba (Emirate Aluminium ACP Simba Fans Player of the Month). Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
Morrison ambaye ni raia wa Ghana amewashinda wachezaji wenzake, mshambuliaji Medie Kagere na kiungo Jonas Mkude ambao aliingia nao fainali.
Morrison amepata kura 2117 sawa na asilimia 46.77, Kagere kura 2117 sawa na asilimia 46.73 na Mkude akipata kura 294 sawa na asilimia 6.50.
Katika mwezi Novemba, Morrison amecheza jumla ya dakika ya 235 akifunga mabao mawili na kusaidia kupatikana kwa mengine mawili.
Post a Comment