Shilole ambaye pia ni mjasiriamali, akizungumza kupitia Wasafi Tv kwenye kipindi cha Big Sunday Live juzi Jumapili, ambapo mtangazaji alimuuliza ikiwa ana ujauzito kufuatia tetesi zinazoendelea mitandaoni zikimuhusisha kuwa kwenye hali hiyo.
“Naona ni kama ndoa imejibu?” Aliuliza mtangazaji. Shilole naye akajibu, “Ya Mungu ni mengi! Kwani naishi na mjomba wako?”.
Alipoulizwa kuhusu umri wa mimba na jinsia ya mtoto mtarajiwa, Shilole alisema atawaambia na kwamba yeye na mumewe (Rommy3d) hawana tabia ya kupima jinsia ya mtoto, hivyo ambaye watajaaliwa watampokea.
Shilole alifunga ndoa na mumewe Rajab Issa maarufu Rommy3d mwezi Aprili mwaka huu, miezi michache baada ya kuachana na mpenzi wake wa awali, Bw Ashraf Uchebe.
Shilole tayari ana watoto wawili wakike, hivyo huyu ajae atakuwa mtoto wake wa tatu na wapili kwa Rommy3d ambaye tayari ana mtoto mmoja wakike mwenye umri wa miaka 2.
Post a Comment