Red Notice imekuwa filamu iliyotazamwa zaidi katika historia ya Neflix.


Red Notice imekuwa filamu iliyotazamwa zaidi katika historia ya Neflix.

Filamu hiyo iliyochezwa na Dwayne John aka The Rock, Ryan Reynolds na Gal Gadot imetazamwa kwa jumla ya masaa milioni 328.8 tangu itoke November 10, Netflix imeripoti.

Kwa namba hizo, imeivunja rekodi ya filamu ya Sandra Bullock, Bird Box ya mwaka 2018 iliyotazamwa kwa masaa milioni 282 ndani ya siku 28.

Hadi sasa asilimia 50 ya subscribers wa Netflix duniani kote wameitazama Red Notice.

Filamu hiyo imetayarishwa na kampuni ya The Rock, Seven Bucks Productions.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post