Ugomvi kati ya mastaa wa bongo kutoka Tanzania, Diamond Platnumz,Harmonize na Alikiba umezidi kuongeza baada ya Harmonize kufichua mambo kadha wa kadha hivi majuzi.
Ni ugomvi ambao umeshuudia na wengi pamoja na mashabiki wao, huku mashabiki wao wakiegemea upande waupendao na kuchukia baadhi ya wasanii.
Professor Jay akiwa kwenye mahijiano, aliwasihi wasanii hao wazike ugomvi wao, kwani utaleta chuki na ugomvi kati ya mashabiki wao.
Jay alizidi na kusema kwamba wamewaachia Mungu, lakini cha muhimu mashabiki wanapaswa kuwaunga wote mkono licha ya ugomvi wao.
"Nimefanya kazi na Diamond na Harmonize na ninawaheshimu. Nimezungumza nao lakini wasiposikiliza basi hakuna tunachoweza kufanya
Tumewaachia Mungu. Ni wao tu wanaoweza kuamua ikiwa hivyo ndivyo wanavyotaka kufuata. Hivi karibuni beef itahamia kwa mashabiki kuchukiana."
Mashindano ya muziki siougomvi, sasa hivi mambo yamekuwa ya kibinafsi. Tutapoteza vipaji vikubwa kwa sababu ya hii beef, sasa hivi tunacheka lakini hii ni beef itaishia pabaya.
Tuwaunge mkono wote, Diamond, Harmonize na Ali Kiba bila kuwa wabinafsi, itakuwa hasara kubwa kumpoteza hata mmoja wao."
Post a Comment