Nandy Akiri Kudharauliwa Tuzo za Afrima




STAA wa Muziki wa Bongo Fleva, Fausta Mfinanga maarufu kama Nandy amefunguka ya moyoni yale aliyoyapitia pindi akiwa nchini Nigeria alipohudhurua hafla ya ugawaji wa Tuzo za Afrima 2021 zilizotolewa usiku wa Novemba 21, 2021.

Akizungumza na waandishi wa habari Nandy amesema, licha ya kukosa tuzo lakini yeye pamoja na mwimbaji mwenzake kutoka Tanzania, msanii Zuchu walionyeshewa dharau na kuchukuliwa poa wa kile alichokiita kutopata ‘treatment’ nzuri.

“Tunalalamika haukuwa wakati sahihi wa kusema wakati ule tunarudi, mtasema kwa sababu tumekosa tuzo sio kwamba hatustahili tuzo, Zuchu anastahili tuzo, mimi nastahili tuzo, kila mtu anastahili pia. Hatupingi kwa ile tuzo waliyompatia binti wa Kenya.

“Lakini kuna ile treatment mtu kuona angalau sijapata tuzo, sijapoteza muda kuna hiki, treatment ambayo nimepata kwa hawa watu ni nzuri ambayo next time nitafikiria kwenda tena, lakini treatment haikuwa nzuri kila mmoja analalamika kivyake.


 
Nandy pia afunguka namna Zuchu na wenzake walivyokosa sehemu yakufikia siku waliyotua Nigeria kushuhudia hafla ya tuzo hizo.

“Mara kina Zuchu wamefika hamna sehemu ya kulala, wameenda kulala sehemu nyingine, yaani na vitu vingine vingine siwezi kuvizungumzia. Zuchu alikuwa kwenye mazoezi, akaja msanii mkubwa wa Nigeria, akaambiwa muda umeisha, lakini Menejimenti yake ipo wazi ikawaambia huyu atamaliza ndio aingie huyo. Ukitoka hapo unajihisi huyo kanionaje, yaani mimi sistahili kufanya mazoezi yangu nikamaliza yakawa mazuri,” aliongeza Nandy.

Hata hivyo mwimbaji huyo anayefanya vizuri kwasasa na kolabo yake na Bill Nas, ataka nini kifanyike ili kuachana na kuwashobokea Wanaigeria. “Tujadili tufanye nini tuache kushoboka na haya mambo ya Nigeria” alimalizia Nandy.

#Udaku Special Blog



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post