Mwijaku Licha ya Kuvutwa Wasafi Atoa Kauli Hii "Siwezi Acha Kumkosoa Diamond Platnumz"



Event kubwa hii leo tarehe 10/12 pale Mlimani City ni uzinduzi wa kampuni ya ubashiri wa michezo, WASAFI BET chini ya @diamondplatnumz ,lakini kubwa zaidi ni kuona @mwijaku_01 ni moja ya mabalozi wa kampuni hiyo.

Kwa mujibu wa Mwijaku amedai mtu wa kwanza kumpigia simu kuhusiana na ishu hiyo alikuwa meneja wa Diamond, @sallam_sk na alipo pokea dili akaangalia linamfaa akazama ndani.

Ishu hii Imekuwa ni trending kwasababu tunaelewa namna Mwijaku anavyo mshambulia, Diamond kwenye mitandao ya kijamii huku akiwa upande wa Harmonize siku zote. Kwa mujibu wa Mwijaku amedai hamtukani Diamond, bali anachokifanya ni kumkosoa kama anavyo kosolewa hata yeye, akiahidi kuwa hatoacha ataendelea kumkosoa siku zote.

Itoshe kusema si kila unaloliona mitandaoni likakujaza sumu, kuna wakati watu wana maisha yenye maelewano tofauti na watu tunavyo fikiria.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post