Mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Maendeleo Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara, Zinati Alifa mkazi wa mtaa wa Mchema mwenye umri wa miaka 13 amebakwa na kisha kuuwawa na maiti yake kutupwa kwenye mapango ya miamba ya Mto kabomola.
Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa huo Shaibu Chande alisema mwili huo uliokotwa ukiwa umetobolewa macho, kabla ya kutokea kwa tukio hilo Septemba 26 mwaka huu majira ya saa 11:30 jioni mwanafunzi huyo aliwaaga wazazi wake kuwa anakwenda kuokota korosho na maembe kwenye mashamba yaliopo maeneo ya Mchemba.
“Mwanafunzi huyo hakurejea hadi usiku ndugu walihofia usalama wake na kuanza kumtafuta bila mafanikio kwa kuwa haikuwa tabia yake, walikwenda hadi kwenye shamba ambalo aliaga anakwenda na hawakumpata”, alisema Chande.
Baada ya juhudi za Ndugu na majirani kumtafuta kwa muda wa siku mbili kutozaa matunda, waliamua kutoa taarifa serikali za mitaa pamoja na Kituo cha Polisi Wilaya ya Masasi. Mpaka kufikia Desemba 1 wasamaria wema walitoa taarifa za kuuona mwili huo majira ya saa 9:00 alasiri na kutokana na mwili kuharibika ulizikwa siku hiyo hiyo saa 10:00 jioni.
Udaku Special Blog
Post a Comment