Mkuu wa Mkoa wa Dar, Amos Makalla "Sijapendezwa na Diamond Platnumz Kukataa Ubalozi wa Mazingira"


Mkuu wa Mkoa wa Dar, Amos Makalla amesema hajapendezwa na tabia ya Diamond ya kukataa kuwa Balozi wa Usafi Dar.

Amesema alitaka Diamond, Alikiba na Harmonize wawe mabalozi wa Usafi katika mkoa wa Dar, Alikiba na Harmonize wamekubali lakini Diamond Platnumz amekataa.

"Mimi kama kaka yao nilitaka niwakutanishe wamalize tofauti zao wawe mabalozi wa Usafi, Alikiba na Harmonize niliwaandikia Barua tu wakakubali, Diamond nilimuandikia Barua na nilimpigia simu akakataa, nimesikitishwa sana"-Makalla.




0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post