Milionea mwenye umri mdogo wa miaka 26, Raia wa New Zealand Jake Millar amefariki Duniani akiwa nchini Kenya katika kifo ambacho kimegubikwa na utata.
Jake amekutwa akiwa amefariki kwenye balcony za nyumba yake eneo la Karen Jijini Nairobi, mwili wake umekutwa ukiwa unaning'inia kwenye kamba na hakukuwa na mwingine zaidi yake Katika eneo hilo.
Polisi wanasema wameambiwa Jake amejiua lakini bado wanaendelea kuchunguza, ni miezi nane imepita tangu Jake aingie Kenya.
Waziri wa Mambo ya Nje wa New Zealand amesema wanapambana kusafirisha mwili na kushughulikia mazishi na taratibu nyingine zitafuata.
#MillardAyoUPDATES
Post a Comment