Kampuni ya kutengeneza roboti ya nchini Urusi inatafuta sura ya binadamu atakayekubali kulipwa ili kuitumia kwenye bidhaa yake mpya ‘Promobot‘.
Kampuni hiyo ya Ulaya, imesema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kwamba iko tayari kulipa $200,000 ambazo ni sawa na zaidi ya shilingi milioni 460 za Kitanzania kwa mtu atakaye kuwa tayari kuipa kampuni hiyo haki ya kuutumia muonekano wa sura yake milele kwenye roboti hilo.
Kampuni hiyo imeweka wazi mpango wao, ambao ni kutumia roboti hiyo mpya yenye sura ya binadamu kama msaidizi katika maeneo yenye shughuli nyingi kama vile hoteli na maduka makubwa.
Kulingana na taarifa waliyoitoa kwa vyombo vya habari, kampuni hiyo imepata mteja ambaye anatazamia kumuweka roboti huyo kama msaidizi katika viwanja vya ndege, maduka makubwa na maduka ya rejareja ifikapo mwaka 2023.
Post a Comment