Meddie Kagere Afunguka Kuhusu Red Arrows na Yanga " Hatutaki Kurudia Tena Makosa"


Mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere amesema michezo miwili mikubwa ijayo ya timu hiyo wanaichukulia kama fainali na watapambana mpaka tone la mwisho uwanjani dhidi ya Red Arrows na Yanga.

Kagere alisema wanatambua uzito kwa kila mchezo ingawa kwa sasa akili zao wamezielekeza kwenye mechi na Red Arrows ili kufanya vizuri na kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

🗣“Kuanzia viongozi, benchi letu la ufundi na wachezaji tumejiandaa vyema kufanya vizuri maana tunatambua umuhimu wa mchezo huo hivyo hatutaki kurudia tena makosa ambayo yalitokea mwanzo,” alisema.

🗣“Kila mchezo kwetu ni fainali, tunajua wengi wanaangalia sana mechi ya Yanga kutokana na ukubwa na historia ya timu hizi lakini tunaenda hatua kwa hatua na zamu yao itafika baada ya kutoka Zambia,” alisema Kagere ambaye ni raia wa Rwanda mwenye asili ya Uganda.

Akiwa na kikosi hicho msimu huu kwenye michezo ya Ligi Kuu Bara amefunga mabao manne kwenye chati ya wafungaji bora nyuma ya kinara wa mabao Jeremiah Juma wa Tanzania Prisons mwenye mabao matano.

Alifunga bao moja kwenye ushindi dhidi ya Dodoma Jiji na Namungo FC huku akitupia mabao mawili kwenye ushindi wa 3-1, dhidi ya Ruvu Shooting.

Tangaza na Udaku Special Blog, piga simu 0714604974


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post