Marekani yaiweka Tanzania katika orodha ya nchi hatari kusafiri





Marekani imeweka Tanzania katika orodha yake ya nchi hatari kusafiri, ikitoa ushauri kwa raia wake kutosafiri katika taifa hilo.

Kituo cha kudhibiti magonjwa nchini Marekani (CDC) imeweka Tanzania katika orodha ya nchi hatari kusafiri.

Kituo hicho kimesema ni vyema kutosafiri katika taifa hilo na kama kuna ulazima basi mtu amepata chanjo kamili dhidi ya corona.

Aidha wamesema, "hali ya sasa nchini Tanzania, hata wasafiri walio na chanjo kamili wanaweza kuwa katika hatari ya kupata na kueneza virusi vipya vya corona" CDC imesema.

Siku ya Jumapili, taarifa zilienea mitandaoni kuwa msafiri kutoka Tanzania alipimwa na kukutwa na aina mpya ya virusi vya corona- Omicron huko New Delhi, India, na kusababisha mamlaka 'kuanza uchunguzi'.

Licha ya tahadhari za mara kwa mara kutoka kwa Wizara ya Afya ya Tanzania, uzingatiaji wa umma kwa hatua za kuzuia Covid-19 bado ukochini, Ubalozi wa Marekani umesema.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post