Staa wa Kenya, #DianaMarua amefunguka kwa mara ya kwanza jinsi muimbaji wa nchini humo, #WillyPaul alivyojaribu kumbaka.
Akiweka video kwenye channel yake ya YouTube, Diana ambaye ni mke wa #Bahati, amesema amelazimika kusimulia mkasa huo baada ya Willy Paul siku za hivi karibuni kumchafua mtandaoni akidai kuwa amewahi kulala naye. Pia anadai ameitukana familia yake, kwa lengo la kutafuta kuongelewa wakati huu ambapo ameachia album yake mpya.
Akiongea huku akizongwa na kilio, Diana amedai kuwa ilimchukua pia miaka mitatu kupata ujasiri wa kumsimulia mumewe tukio hilo la aibu.
Amesema miaka kadhaa iliyopita, Willy Paul alikuwa akimtongoza kiasi ambacho iligeuka kuwa kero kwa Diana. Hata hivyo amesimulia kuwa siku moja Willy alimuomba wazungumze na kumuita kwenye gari lake. Aliamua kumkubalia ili amsikilize tu.
#Diana alipoingia kwenye gari hilo, Willy alifunga milango na kuweka muziki kwa sauti kubwa na kuendesha gari kwa spidi kama mwendawazimu. Walipofika karibu na nyumbani kwake alimuambia waingie kwake, Diana aligoma na ndipo Willy akageuka mbogo na kumparamia, kumkaba na kurarua nguo zake.
Diana anasema alipambana naye huku akipiga kelele kwa nguvu na bahati akapanick, kitendo kilichompa upenyo wa kufungua mlango na kukimbia.
Mrembo huyo ambaye naye ameingia kwenye muziki siku za hivi karibuni, ameapa kumpeleka mahakamani Willy Paul kwakuwa ni wanawake wengi aliowafanyia ukatili huo na kwamba ni lazima awamu hii sheria ichukue mkondo wake.
Mtazame Kwenye VIDEO Hii:
Post a Comment