Events zote zimefanyika Jana Jijini Dar Es Salaam. Komaa Concert imefanyika Pande za Kawe na Bata la Dar pande za Leaders.
Show zote zilikuwa ni Bure, hakukuwa na kiingilio.
Kwa walioshuhudia show zote lazima watakubaliana na mimi kuwa, Komaa concert imetisha sana kuliko Bata la Dar, kiukweli Majizzo anastahili pongezi kubwa, hii inaonesha ushupavu wake na umakini mkubwa katika kazi.
Hata Wasanii Waliohudhuria katika Komaa Concert wamekubali kuwa show ilikuwa ni moto. Nandy, The African Princess amekiri kabisa kwamba ndani ya mwaka huu katika Shows kubwa ambazo amefanya basi na Komaa Concert Ipo kwenye list.
Kubuma kwa Bata la Dar inaonesha ni jinsi gani Clouds Media imepoteza mvuto kwa watanzania, hivi inakuaje leo hii media changa kama Efm inaandaa Event na inakuwa kubwa kuliko Event ya Media yenye Miaka zaidi ya Ishirini kwenye Game, hii ni aibu kubwa, Watu wengi sana wamehudhuria KOMAA CONCERT na Watu wachache sana wamehudhuria BATA LA DAR. Clouds Media inabidi ijitathimini kupitia hili. Huenda waendako sipo, wanapotea njia.
Kuna haja ya Clouds Media kufanya Mabadiriko ya kiutawala ndani ya muda mfupi sana, Clouds Media Imeshindwa kusimama kabisa baada ya Kifo cha Mtaalamu Ruge Mutahaba.
Hakika, Clouds Media imekosa mtu wa kuziba pengo la Ruge. Mbali na Clouds Media, mwenye Kariba ya Ruge ni mmoja tu kwasasa, naye ni Majizzo, hivyo majizzo ataendelea kuwaburuza sana CloudsMedia kama hawatapata muarobaini wa matatizo yao.
Post a Comment