Rappa #RosaRee ameipinga vikali kauli hii ya rappa #Wakazi kuhusu wasanii wa Hip Hop nchini akisema kwamba wamepoteza mvuto wa kibiashara hivyo ni ngumu kwa wawekezaji kuwadhamini. Akiongeza kuwa wamekosa weledi na uwezo wa kibiashara nyuma ya wasanii wa Singeli na Bongo fleva.
Kauli hii #Wakazi aliitoa kufuatia shabiki mmoja kupendekeza kwamba anatamani kufanyika kwa onesho kubwa la Hip Hop Desemba hii.
Leo, Alhamisi, Desemba 2, rappa #RoseRee ametumia ukurasa wake wa instagram kumjibu Wakazi kuhusu kauli yake aliyoitoa juu ya wanamuziki wa Hip Hop nchini, Rosa ameeleza kuwa haiungi mkono kauli ya “Wana HipHop” wamekosa mvuto wa kibiashara, kwani kuna wengine wanapata madili kibao, yeye akiwemo.
"Kwa kweli hapa @wakazi sijakuunga mkono. Siamini kama haya Ndio majibu yako kwa mtu ambaye anaipenda Hip Hop na kujua value yake mpaka anatamani kuwe na tamasha la Hip Hop. Kuna umuhimu wa kuona juhudi zinazofanyika na wanaHipHop out here kuweka game afloat. Ni dhahiri kwamba bado tunahitaji kufanya kazi kubwa kuweza kuikuza HipHop ila ukisema kwamba “Wana HipHop” wamekosa mvuto wa kibiashara unakosea maana wengine tunapata madili kibao. As of now personally I’m working with Darling, Coca-Cola, JohnnieWalker na we’re in talks many others.
Hatuwezi kusema kwamba kila mwaka tunasubiria deal za kampuni moja na wasipotupa deal Basi Hip Hop haipo. Lazima tujiongeze na tuwe flexible enough kufanya kazi na watu wengi. And kuna wana HipHop wengine wanaofanya vizuri pia kwenye industry we can’t overlook that. Tukifanya juhudi zetu binafsi then wote tukafanya juhudi za umoja then ndo tutaiendeleza HipHop zaidi. Ila kukiwa kuna wanaHipHop ambao labda wamepunguza speed ya game sio haki kusema kwamba HipHop kiujumla imelala au haipo au “imepoteza mvuto wa kibiashara”…..
Tufanye juhudi za peke yetu then tufanye za kiujumla kuikuza HipHop. Tutoe magoma makali, tuwaburudishe mashabiki kupitia platform zetu, tuwafikirishe kwenye mashairi, tupendeze, tupige picha kali, TUFANYE KAZIIIII. Hakuna kampuni inayoweza kufanya kazi na mtu yeyote (sio kwenye HipHop tu) ambaye hataiongeza kampuni katika namna flani au nyingine, na pia hatuwezi tukawaongezea makampuni kama hatujiongezi sisi wenyewe Kwanza! Ukipata Value personally Ndio utaweza kuipa kampuni Value pia. Let’s us make personal efforts then we join them to make general efforts.” - ameongeza Rosa Ree.
Una mtazamo gani kwenye hili⁉️
Post a Comment