Kocha wa Chama: Yanga Inawafunga Simba





KOCHA Mkuu wa RS Berkane ya Morocco, Florent Ibenge, ameitabiria Yanga kuondoka na ushindi mbele ya Simba katika mchezo wa dabi ya Kariakoo utakaochezwa leo Jumamosi katika Uwanja wa Mkapa,
Dar.


Ibenge ambaye aliwahi kuwa Kocha Mkuu wa AS Vita na timu ya taifa ya DR Congo, analifahamu vyema soka la
Tanzania akiwa amewahi kukutana na Simba na Taifa Stars.


Kocha huyo ndiye anayewafundisha viungo wa zamani wa timu hizo, Clatous Chama na Tuisila Kisinda.
Ibenge aliliambia Championi Jumamosi kuwa anauona mchezo ukiwa mgumu kwa timu zote huku akiipa nafasi Yanga ya kuibuka na ushindi kutokana na kuwa na mwanzo mzuri wa ligi pamoja na kufanya usajili mzuri ambao umewasaidia kuwa bora.


“Mchezo utakuwa mgumu kwa kuwa ni mchezo wa dabi. Simba nimekutana nao mara kwa mara nikiwa na AS Vita, mara zote nimewaona wakiwa bora lakini kwa sasa hawapo vizuri sana, kuna kitu kimepungua kwao, jambo
ambalo naamini litakuwa faida kwa Yanga.


“Yanga wameanza vizuri katika ligi, usajili ambao wameufanya umekuwa bora kwao na umewafanya kuonekana katika muundo mzuri wa timu wakiwa na faida ya maelewano ya haraka, hivyo kama watafanikiwa kuwa katika ubora wao naamini watapata ushindi mbele ya Simba,” alisema Ibenge.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post