WAENDESHA mashtaka katika kitongoji cha Detroit wamemfungulia mashtaka ya ugaidi na mauaji ya kukusudia mvulana wa miaka 15 anayetuhumiwa kuwafyatulia risasi na hatimaye kuwaua wanafunzi wenzake wanne katika Shule ya Upili ya Oxford.
Mvulana huyo, Ethan Crumbley, anashtakiwa kama mtu mzima, alisema Karen D. McDonald, mwendesha mashtaka wa Kaunti ya Oakland siku ya Jumatano, Dis. 1.
Mbali na makosa manne ya mauaji ya daraja la kwanza na moja la ugaidi kwa kusababisha kifo, Crumbley anakabiliwa na makosa saba ya kushambulia kwa nia ya kuua na makosa 12 ya kupatikana na bunduki katika kutekeleza uhalifu.
McDonald amesema pia anazingatia mashtaka dhidi ya wazazi wa mshukiwa, ambao walikuwa na mkutano wa ana kwa ana na maafisa wa shule siku ya Jumanne – takriban saa tatu kabla ya kupigwa risasi – kuhusu tabia ya mshukiwa darasani, kulingana na askari wa Kaunti ya Oakland, Michael Bouchard.
Udaku Special Blog
Nafasi za Ajira Bonyeza www.ajirayako.co.tz
Post a Comment