Kanye West ameweka wazi kuwa anajaribu kumrudisha mke wake. Hata hivyo, bado inaonekana Kim Kardashian ana mpango mbadala kwenye mahusiano hayo na Ye.
Kwa mujibu wa TMZ, Kim anasonga mbale katika harakati za kuachana na Kanye, na ili mchakato uende haraka zaidi, inasemekana amefungua kesi ya kudai kuachana kihalali.
Nyaraka hizo ziliripotiwa kuwasilishwa Ijumaa Desemba10, 2021, Kim amemuomba jaji kutenganisha masuala ya malezi ya watoto na mali za wanandoa hao na pia ameomba kurejeshewa jina lake la ukoo badala ya kutambulika kwa jina la mumewe la West.
Habari hizi zinakuja saa chache baada ya Kanye kubadilisha mashairi kwenye wimbo wake ‘Runaway’ ambapo alisema, “Run back to me” huku ikitafsiriwa kuwa kauli hiyo ilimlenga Mkewe huyo kwa kumtaka Kim amrudie pale alipomtaja Kim kwa jina lake halisi ‘Kimberly’
Post a Comment