JE, Diamond Platnumz Ana Donge na RC Makalla?



UKISIKIA “donge” maana yake kinyongo yaani ile chuki nzito juu ya mtu fulani aliyekufanyia ndivyo sivyo.

Sasa bwana tangu habari za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla kulalamikia “mgomo” wa Msanii Diamond kushiriki katika kampeni ya usafi aliyoizundua licha ya kumwalika kwa simu na barua, mambo yamekuwa mengi kwenye mitandao ya kijamii.

Za ndani ila nyepesinyepesi zilizojaa hisia za kibinadamu zinaeleza kuwa eti msanii huyo hakushiriki kwenye kampeni hiyo licha ya kupewa mwaliko kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ana kinyongo na RC Makalla kutokana na ile kauli yake ya kumsifia msanii mwenzake Ali Kiba kwamba anatunga nyimbo zenye maadili; nafikiri unaikumbuka.

Kweli Diamond awe na kinyongo na mkuu wa mkoa? Aaah jamani hebu temeeni mate chini.


Bora hata kuamini wanaodai kuwa, hakufika kwenye kampeni hiyo kwa sababu alitaka kukwepa mtego wa “upatanisho” kati yake na Ali Kiba uliokuwa umesetiwa na RC Makalla au nafuu hata kuamini kuwa Mondi alikuwa bize; lakini kumsingizia kinyongo, sijui bwana labda wewe unaelewa zaidi!

By @manyota_rich


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post